Ibara 6
Ufafanuzi
Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali
Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.