Wakili Msomi

Ibara 102

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka yake

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar · Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Zanzibar

(1)Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(2)Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii na katika ibara zifuatazo katika Sura hii ya Katiba hii, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaundwa na itatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1980 Na.45 ib.55: na Sheria ya 1984 Na.15 ib.14: Sheria ya 1994 Na.34 ib.16

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.