Ibara 103
Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na madaraka yake
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar · Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Zanzibar
(1)Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
(2)Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanizibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984.
(3)Pamoja na madaraka yake mengine kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndiye atakayewateua na kuwakabidhi madaraka Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1980 Na.15 ib.14 1994 Na.34 ib.17
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.