Wakili Msomi

Ibara 107

Madaraka ya Baraza la Wawakilishi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar · Baraza la Wawakilishi la Zanzibar

(1)Rais wa Zanzibar kama sehemu moja ya Baraza la Wawakilishi la atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii na pia Katiba ya Zanzaibar kwa ajili hiyo.

(2)Wajumbe wawakilishi kama Baraza la Wawakilishi watakuwa ndicho chombo kikuu cha Tanzania Zanzibar ambacho kitakuwa na madaraka kwa lniaba ya wananchi wa Tanzania Zanzibar, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vyombo lvyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar.

(3)Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Baraza la Wawakilishi laweza -

(a)kumuuliza Waziri yeyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Tanzania Zanzibar yaliyomo katika wajibu wake;

(b)kujadili utekelezaji wa kila Wizara ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa Mkutano wa Baraza la wawakilishi wa kila mwaka wa bajeti;

(c)kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa Tanzania Zanzibar, na kutnga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;

(d)kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;

(e)kutayarisha au kuagiza itayarishwe na kuwasilisha kwenye Chama taarifa kuhusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15; ib.20

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.