Wakili Msomi

Ibara 54

Baraza la Mawaziri

Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri na Serikali

(1)Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

(2)Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza Mikutano hiyo.

(3)Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

(4)Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.

(5)Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ibara 9 Sheria Na.4 ya 1992 ib… Sheria Na.34 ya 1994 ibara 12

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.