Ibara 60
Katibu wa Baraza la Mawaziri
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri na Serikali
Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri ambaye atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri, na atatekeleza shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumla au maalum atakayopewa na Rais, yaani:
(a)kuanda ratiba ya mikutano ya Baraza na kutayarisha orodha ya shughuli za kila mkutano;
(b)kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza;
(c)kutoa taarifa na maelezo ya maamuzi ya Baraza kwa kila mtu au chombo cha umma kinachohusika na uamuzi wowote; na
(d)kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozote atakazoagizwa mara kwa mara na Rais.
Marejeo ya marekebisho: sheria ya 1984 Na.15 ib. 9
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.