Ibara 55
Uteuzi wa Mawaziri
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri na Serikali
(1)Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(2)Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.
(3)Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambao watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.
(4)Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.
(5)Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ibara 9
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.