Ibara 88
Sekretariati ya Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge
(1)Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa na nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa idadi atakayoagiza Rais.
(2)Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi na ngazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume ya Utumishi inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge.
(3)Sekretariati ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge itaendeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa Bunge na wa Wabunge wa madaraka ya Bunge chini ya Katiba hii.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.