Wakili Msomi

Ibara 89

Kanuni za Kudumu za Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge

(1)Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.

(2)Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli za Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bunge ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.14 ib.14

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.