Ibara 101
Kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa majadiliano na wa shughuli
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge
Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuwezesha mahakama na sheria kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu wa shughuli katika Bunge ambao kwa mujibu wa ibara ya 100 umedhaminiwa na Katiba hii.
Marejeo ya marekebisho: sheria ya 1984 Na.15 ib.14
Ibara 100Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuliIbara 102 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka yake
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.