Wakili Msomi

Ibara 100

Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge

(1)Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2)Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.