Ibara 94
Kiwango cha vikao vya Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge
(1)Kiwango cha kila kikao cha Bunge ni nusu ya Wabunge wote.
(2)Isipokuwa kama imeelezwa vingine katika Katiba hii, kila swali litakalotolewa kwa ajili ya kupata uamuzi wa Bunge litaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura za Wabunge waliohudhuria na kupiga kura.
(3)Spika, Naibu wa Spika, au mtu mwingine atakayeongoza kikao cha Bunge, hatakuwa na kura ya kawaida bali atakuwa na kura ya uamuzi kukitokea usawa wa kura.
(4)Kanuni za Bunge zaweza kuweka masharti kwamba Mbunge yeyoyote atakayepiga kura juu ya jambo lolote ambalo yeye binafsi ana masilahi nalo atahesabiwa kuwa hakupiga kura.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.