Wakili Msomi

Ibara 95

Viti vilivyo wazi katika Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge

Bunge laweza kutekeleza shughuli wakati wa vikao vyake bila ya kujali kwamba kuna kiti kilicho wazi miongoni mwa viti vya Wabunge (iwe kiti hicho kimekuwa wazi tangu Bunge lilipokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au kimekuwa wazi baada ya Mkutano huo wa kwanza) na iwapo katika shughuli hizo atashiriki mtu yeyote ambaye hana haki ya kushiriki au kama wakati wa shughuli hizo atakuwapo mtu yeyote ambaye hana haki ya kuwapo, basi kushiriki kwa mtu huyo au kuwapo kwake hakutabatilisha shughuli hizo.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.