Wakili Msomi

Ibara 92

Mikutano ya Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge

(1)Bunge litafanywa mikutano yake mahali ambapo ni desturi kufanya Mikutano hiyo au mahali pengine popote katika Jamhuri ya Muungano patakapotajwa na Rais kwa ajili hiyo.

(2)Mkutano wa kwanza wa Bunge katika Maisha ya Bunge utaanza siku ile ambayo Bunge limeitwa kukutana, na kila Mkutano ufuatao utaanza siku yoytote itakayopangwa na Bunge lenyewe au siku yoyote itakayopangwa kwa mujubu wa Kanuni za Bunge.

(3)Rais aweza kuitisha Mkutano wa Bunge wakati wowote.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.