Ibara 93
Uongozi wa vikao vya Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge
Kila kikao cha Bunge kitaongozwa na mmojwawapo wa watu wafuatao, yaani-
(a)Spika au;
(b)ikiwa Spika hayupo, Naibu wa Spika, au
(c)ikiwa Spika na Naibu wa Spika wote hawapo, Mbunge yeyote aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo, lakini Waziri, au Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina yingine yoyote iliyotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya ibara hii hataweza kuchaguliwa kwa mujibu wa mahsarti ya aya hii.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.14
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.