Wakili Msomi

Ibara 86

Utaratibu wa kumchagu Spika na Naibu wa Spika

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Utaratibu, Madaraka na Haki za Bunge

(1)Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Spika.

(2)Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu wa Spika wakati wo wote katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya utakaoteuliwa na Bunge na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge mara baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Naibu wa Spika.

(3)Uchaguzi wa Spika, na vile vile uchaguzi wa Naibu wa Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.