Wakili Msomi

Ibara 62

Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Bunge

(1)Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.

(2)Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katika ibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge.

(3)Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hii au masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile vile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.12

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.