Wakili Msomi

Ibara 76

Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Wabunge, Wilaya ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Wabunge

(1)Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.

(2)Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.

(3)Bila ya kujali masharti ya ibara hii yaliyotangulia, ifahamike kwamba ikiwa tarehe ya kuvunjwa Bunge imetangazwa au inafahamika kutokana na matukio yaliyoelezwa katika ibara ndogo ya (3) ya ibara ya 90, basi uchaguzi wa namna hiyo hautafanywa katika kipindi chote cha miezi kumi na mbili ya nyuma ikihesabiwa tangu tarehe hiyo.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib. 13 Sheria ya 2000 Na.3 ib.15

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.