Wakili Msomi

Ibara 105

Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar · Baraza la Mapinduzi la Zanzibar

(1)Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na wajumbe wafuatao:

(a)Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;

(b)Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;

(c)Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;

(d)Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar.

(2)Bila ya kuyaingilia madaraka ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kama kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake ya uongozi na usimamizi wa shughuli za Serikali ya Zanzibar na pia utekelezaji wa madaraka yake juu ya shughuli zote za Serikali kuhusu mambo yote yasiyo mambo ya Muungano, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na yale ya Katiba ya Zanizbar.

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.