Wakili Msomi

Ibara 104

Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar · Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Zanzibar

(1)Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla au uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

(2)Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utafanyika ili kujaza nafasi hiyo kila mara litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo.

(a)baada ya Baraza la Wawakilishi kuvunjwa;

(b)baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujiuzulu bila ya kulivunjwa Baraza la Wawakilishi kwanza;

(c)baada ya kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupoteza sifa za kushika nafasi ya madaraka ya kuchaguliwa;

(d)baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushtakiwa katika Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1984 na kuondolewa katika madaraka.

(e)baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1984 kwamba Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawezi kumudu kazi na shughuli zake;

(f)baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufariki.

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.