Ibara 107A
Mamlaka ya Utoaji Haki
Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano
(1)Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.
(2)Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a)kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi;
(b)kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c)kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge;
(d)kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro;
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 2000 Na.3 ib.17
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.