Wakili Msomi

Ibara 115

Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar

Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama Kuu ya Zanzibar

(1)Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 83 na 116 ya Katiba hii, mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar yatakuwa kama itakavyoelezwa katika Sheria zinazotumika Zanzibar.

(2)Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge, iwapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inayotumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Visiwani imekabidhi madaraka yoyote kwa Mahakama Kuu, basi Mahakama Kuu ya Zanzibar yaweza kutekeleza madaraka hayo kwa kiasi kile kile inavyoweza kutekeleza Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1985 Na.15 ib.22 na 25

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.