Wakili Msomi

Ibara 108

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake

Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano

(1)Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu") ambayo mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.

(2)Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi kwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanza katika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la aina hiyo. Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za kisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu.

Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1979 Na.14 ib.6

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.