Ibara 7
Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili
Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali
(1)Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii ya Sura hii.
(2)Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama sheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti ya Sehemu hii ya Sura hii.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.