Ibara 138
Masharti ya kutoza kodi
Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano
(1)Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria na sheria iliyotungwa na Bunge.
(2)Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii hayatalizuia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kutumia mamlaka yake ya kutoza kodi ya aina yoyote kwa mujibu wa madaraka ya Baraza hilo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.43
Ibara 137Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya SerikaliIbara 139 Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria ya matumizi kuanza kutumika
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.