Ibara 139
Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria ya matumizi kuanza kutumika
Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano
(1)Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
(2)Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali inayohusika na mwaka huo haijaanza kutumika basi Rais aweza kuidhinisha fedha itolewe kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya kulipia gharama za lazima za shughuli za Serikali, na fedha hizo zitatumiwa mpaka ipite miezi minne tangu mwanzo wa mwaka wa fedha mpaka Sheria ya matumizi ya Fedha za Serikali itakapoanza kutumika, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo litakalotokea mapema zaidi.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.43
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.