Ibara 65
Muda wa Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Bunge
(1)Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.
(2)Kwa madhumuni ya Katiba hii maneno "maisha ya Bunge" maana yake ni ule muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge jipya limeitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaida kufanyika.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.12
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.