Wakili Msomi

Ibara 43

Masharti ya kazi ya Rais

Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Rais

(1)Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2)Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.