Ibara 44
Madaraka ya kutangaza vita
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Rais
(1)Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2)Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita lililotolewa na Rais.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9 Sheria ya 1992 Na.4 ib.14
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.