Ibara 141
Deni la Taifa
Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano
(1)Deni la Taifa litadhaminiwa na Mufko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2)Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara hii deni la Taifa maana yake ni deni lenyewe na pia faida inayolipwa juu ya deni hilo, fedha zinazowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni pole pole na gharama zote zinazoambatana na usimamizi wa deni hilo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.43
Ibara 140Mfuko wa Matumizi ya dharuraIbara 142 Mishahara ya watumishi fulani wa Serikali kudhaminiwa na Mfuko Mkuu Wa Hazina ya Serikali
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.