Wakili Msomi

Ibara 133

Akaunti ya Fedha ya Pamoja

Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mchango na Mgawanyo wa Mapato ya Jamhuri ya Muungano

Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akauti maalum itakayoitwa "Akaunti ya Fedha ya Pamoja" na ambayo itakuwa ni sehehmu ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambamo kutawekwa fedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi kitakachoamuliwa na Tume ya pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.42

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.