Wakili Msomi

Ibara 134

Tume ya Pamoja ya Fedha

Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mchango na Mgawanyo wa Mapato ya Jamhuri ya Muungano

(1)Kutakuwa na Tume ya pamoja ya Fedha yenye wajumbe wasiozidi saba ambao watateuliwa na Rais kwa mujibu wa ibara hii na masharti ya sheria iliyotungw na Bunge.

(2)Majukumu ya Tume yatakuwa ni:

(a)kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano, na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango na mgawo wa kila mojawapo ya Serikali hizo;

(b)kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili;

(c)kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.42

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.