Ibara 135
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Masharti Kuhusu Fedha za Jamhuri ya Muungano · Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano
(1)Fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa fedha za aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, zitawekwa katika mfuko mmoja maalum ambao utaitwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
(2)Fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na Sheria kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.
Ibara 134Tume ya Pamoja ya FedhaIbara 136 Masharti ya kutoa fedha za matumizi kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.