Wakili Msomi

Ibara 123

Mashauri yanayoweza kuamuliwa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani

Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano

Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani aweza kutekeleza madaraka yoyote ya Mahakama ya Rufani ambayo hayahusiki na kutoa uamuzi juu ya Rufaa:

Isipokuwa kwamba:

(a)Katika mashauri ya jinai, iwapo Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeombwa kutekeleza madaraka hayo atatoa uamuzi ambao mwombaji haridhiki nao, basi mwombaji atakuwa na haki kutaka maombi yake yaamuliwe na Mahakama ya rufani;

(b)Katika mashauri ya madai, Mahakama ya Rufani yaweza kubatilisha au kubadilisha amri, agizo au uamuzi wa namna nyingine wowote uliotolewa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

Marejeo ya marekebisho: Sheria za 1979 Na.14 ib.8 na Sheria ya 1984 Na.15 ib.33

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.