Ibara 122
Kiwango cha vikao vya Mahakama ya Rufani
Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano
(1)Kiwango cha kila kikao cha Mahakama ya Rufani ni Majaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua watatu.
(2)Katika kila rufaa suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama ya Rufani litaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani waliosikiliza rufaa.
Marejeo ya marekebisho: Sheria za 1979 Na.14 ib.8 na Sheria ya 1984 Na.15 ib.32
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.