Ibara 119
Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani
Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano
Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri lolote katika Mahakama Kuu au katika Mahakama ya Hakimu ya ngazi yoyote:
Isipokuwa kwamba iwapo Jaji yeyote wa Mahakama Kuu atateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi hata baada ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji huyo aweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama Kuu mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, na kwa ajili hiyo itakuwa halali kwake kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote unaohusika kwa kwa kutumia na kutaja madaraka aliyoshika kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, lakini endapo hatimaye hukumu hiyo au uamuzi huo mwingine utapangwa kwa njia ya rufaa itakayofikishwa mbele ya Mahakama ya Rufani, basi katika hali hiyo Jaji huyo wa Mahakama ya Rufani, hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria za 1979 Na.14 ib.8 na 1984 Na.14 ib.29
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.