Wakili Msomi

Ibara 69

Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya Viongozi

Bunge la Jamhuri ya Muungano · Wabunge, Wilaya ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Wabunge

(1)Kila Mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama Mbunge kuwasilisha kwa Spika nakala mbili za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67.

(2)Tamko rasmi linalotakiwa kuwasilishwa kwa Spika kwa mujibu wa masharti ya ibara hii litatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(3)Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja ya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(4)Katika ibara hii na katika ibara ya 70 na ya 84 "Kamishna wa Maadili" maana yake ni Kamishna aliyeteuliwa kuwa kiongozi wa Sekretariati ya Maadili iliyotajwa katika ibara ya 132 ya Katiba hii.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1995 Na.12 ib.11

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.