Ibara 70
Wabunge kutoa taarifa ya mali
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Wabunge, Wilaya ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Wabunge
(1)Kila Mbunge atatakiwa kuwasilisha kwa Spika nakala mbili za taarifa rasmi ya maelezo ya mali yake na kadri itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Taarifa itatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na itatolewa mara kwa mara kama itakavyoagizwa na Sheria hiyo.
(2)Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja ya kila taarifa rasmi iliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti ya ibra hii.
(3)Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kwa makusudi ya kusimamia hifadhi ya taarifa ya mali iliyowasilishwa na Mbunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, na kuhakikisha kwamba watu wasioruhusiwa au wasiohusika hawapati nafasi ya kuona taarifa ya mali wala kujua yaliyomo katika taarifa ya mali.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1995 Na.12 ib.12
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.