Ibara 40
Haki ya kuchaguliwa tena
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Rais
(1)Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho.
(2)Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais.
(3)Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Zanzibar.
(4)Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9 Sheria Na.34 ya 1994 ib.9
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.