Wakili Msomi

Ibara 39

Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais

Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Rais

(1)Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(a)ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.

(b)ametimiza umri wa miaka arobaini;

(c)ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(d)anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,

(e)katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

(2)Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kama si mwananchama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1992 Na.4 Sheria ya 1994 Na.13 ib… Sheria ya 1994 Na.34 ib…. Sheria ya 2000 Na.3 ib.7

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.