Ibara 35
Utekelezaji wa shughuli za Serikali
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Rais
(1)Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais.
(2)Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
Ibara 34Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yakeIbara 36 Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.