Ibara 52
Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano · Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri na Serikali
(1)Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2)Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
(3)Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.