Ibara 3
Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi
Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea · Jamhuri ya Muungano na Watu
(1)Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2)Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1992 Na.4 ib.5
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.