Ibara 147
Marufuku kuunda majeshi ya ulinzi yasiyo majeshi ya ulinzi ya Umma
Majeshi ya Ulinzi
(1)Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2)Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania.
(3)Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4)Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.49 Sheria ya 1992 Na.4 ib.36
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.