Wakili Msomi

Ibara 146

Kazi za Serikali za Mitaa

Madaraka ya Umma

(1)Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.

(2)Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo -

(a)Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo lake;

(b)Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na

(c)Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.20

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.