Ibara 145
Serikali za Mitaa
Madaraka ya Umma
(1)Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.
(2)Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.50
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.