Ibara 127
Muundo wa Mahakama Maalum ya Katiba
Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
(1)Mahakama Maalum ya Katiba itakuwa na wajumbe ambao nusu ya jumla ya wajumbe wote watateuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na nusu nyingine ya jumla hiyo watateuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(2)Mtu anayeweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Mahakama Maalum ya Katiba ni yule tu ambaye ni jaji au aliyepata kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar, au mtu mwenye uwezo na ujuzi wa kazi ya Jaji na anayestahili kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji kwa mujibu wa Sheria inayotumika Tanzania Bara na sheria inayotumika Tanzania Zanzibar, kadri hali itakavyokuwa.
(3)Mtu aweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Mahakama Maalum ya Katiba ama kwa ajili ya kusikiliza shauri moja tu au mashauri mawili au zaidi kama yatatokea. Mjumbe ataendelea kutekeleza madaraka ya kazi yake kama Mjumbe wa Mahakama Maalum ya Katiba mpaka shauri analohusika nalo litakapokwisha au mpaka uteuzi wake utakapofutwa au mpaka atakaposhindwa kutekeleza kazi yake kama Mjumbe kwa sababu ya maradhi au sababu nyingine yoyote.
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1984 Na.15 ib.37
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.