Wakili Msomi

Ibara 126

Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba

Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano

(1)Kazi pekee ya Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni kusikiliza shauri lililotolewa mbele yake, kutoa uamuzi wa usuluhishi, juu ya suala lolote linalohusika na tafsiri ya Katiba hii iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

(2)Katika kutekeleza kazi yake kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Mahakama Maalum ya Katiba haitakuwa na mamlaka ya kuchunguza au kubadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu au uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 83 ya Katiba hii au uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kwa mujibu wa ibara ya 117 ya Katiba hii.

(3)Kila uamuzi wa usuluhishi utakaotolewa na Mahakama Maalum ya Katiba kwa mujibu wa ibara hii utakuwa ndio wa mwisho, hakutakuwa na haki ya kukata rufaa popote.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1979 Na.14 ib.9 na Sheria ya 1984 Na.15 ib.36

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.