Wakili Msomi

Ibara 112

Tume ya Kuajiri ya Mahakama

Utoaji Haki katika Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Tume ya Kuajiri ya Mahakama ya Tanzania Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano · Madaraka ya Kuajiri Mahakimu na Watumishi Wengine wa Mahakama za Tanzania Bara na Tume ya Kuajiri ya Mahakama

(1)Kutakuwa na Tume ya Kuajiri kwa ajili ya Mahakimu na Watumishi wengineo wa Mahakam za Tanzania Bara. Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa hawa wafuatao:-

(a)Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti;

(b)Mwanasheria Mkuu;

(c)Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ambaye atateuliwa kwa ajili hiyo na Rais baada ya kushauriana na Jaji Mkuu

(d)Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu;

(e)Wajumbe wawili ambao watateuliwa na Rais.

(2)Mtu hataweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii ikiwa mtu huyo ni Mbunge au ni mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote iliyotajwa kwa ajili hiyo na sheria iliyotungwa na Bunge.

Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1985 Na.15 ib.22 Sheria ya 1990 Na.14 ib.6

Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.