Ibara 81
Utaratibu wa kupendekeza majina ya wagombea uchaguzi wa Wabunge Wanawake
Bunge la Jamhuri ya Muungano · Wabunge, Wilaya ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Wabunge
Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibu utakaotumiwa na vyama vya siasa kwa ajili ya kuchagua na kupendekeza majina ya Wabunge wa aina iliyotajwa katika ibara ya 66(1) (b).
Marejeo ya marekebisho: Sheria ya 1992 Na.4 ib.29
Source: official text. If anything here differs from the official publication, the official publication prevails.